Rapper asieishiwa vituko na matukio Curtis Jackson a.k.a 50 Cent,alfajiri ya kuamkia June 27 alijikuta akiwa mikononi mwa polisi,akishikiliwa kwa kosa la kutamka lugha ya matusi mbele ya hadhira wakati aki-perfom kwenye mji wa St.Kitts,uliopo pwani ya visiwa vya Caribbean weekend hii.
Inadaiwa kuwa 50 Cent,alitaamka neno “motherf*cker,”wakati aki-perfom wimbo wake wa ‘P.I.M.P’ akiwa ameshika kipaza sauti huku akijua wazi kuwa DJ wake hakuwa na ‘clean version’ (mashairi yaliyohaririwa) ya wimbo huo.
Hata hivyo rapper huyo aliruhusiwa kumaliza show yake,ambapo iliwabidi polisi wamsubiri ashuke stejini huku taarifa za awali zikidai kuwa kutokana na kitendo hicho atakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu ‘misdemeanor charge’.
Hatua hii inaweza kuwa funzo kwa wanamuziki wengine hata hapa nyumbani,hasa wale wanaopenda kutoa lugha za matusi au zenye kuudhi wakiwa stejini bila kujali mashabiki wao wanaathirika kiasi gani na matamshi ya aina hiyo.


No comments:
Post a Comment