Hatimaye baada ya
matukio ya moto kuikumba Wilaya ya Karagwe mara kwa mara na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo
kutokana na kutokuwa na gari la Zimamoto uongozi wa Wilaya hiyo kupitia Mkuu wa Wilaya Mhe.
Deodatus Kinawilo ulifanikisha juhudi za kupata gari la kuzima moto wakati
janga hilo linapotokea.
Gari hilo lilitolewa na
Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto nchini na lilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Juni 8, 2016 katika viwanja
vya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na kurikabidhi kwa Mkuu wa Kituo cha
Wilaya cha Jeshi la Zimamoto na Uokozi Karagwe Sajenti P.F. Mmbale tayari kwa
ajili kukabiliana na majanga ya moto.
Pamoja na gari hilo
kutoka nchini Japani kuzinduliwa lakini kimuundo limetengenezwa kwa ajili ya
kazi za uokoaji pamoja na kuzima moto maeneno ambayo yana vyanzo vya maji kama
‘fire hydrant’, visima vikubwa, mabwawa pamoja na sehemu ambazo gari kubwa za
zimamoto hazifiki kwa hiyo kutokana na
mazingira ya Wilaya ya Karagwe kutokuwa miundombinu hiyo ya maji gari
linahitaji kuboreshwa.
Maboresho hayo ni
pamoja na kuwa na msaada wa kuwepo na gari linalobeba maji safi (water bowzer)
pindi tukio la moto likitokea bowzer na gari la zimamoto yaongozane kutoa
msaada wa maji wakati wa kuzima moto. Au gari la zimamoto lijengewa tanki la
maji kulingana na uwezo wake angalau lita 2000 kwani gari hilo lilikuwa halikutengenezwa kwa lengo la kubeba maji bali ni (Movable Pump).
Baada ya Mkuu wa Mkoa
kupokea taarifa na kuonekana kuwa gari hilo pamoja na kuzinduliwa lakini ili
liweze kufanya kazi linahitaji kuboreshwa na kulikuwa kunahitajika kiasi cha
shilingi milioni (20,000,000/=) Mhe.
Kijuu aliamua kuendesha harambee ambapo wadau mbalimbali na watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Karagwe kwapamoja walichangia
katika harembee hiyo.
Katika harambee hiyo
zilipatikana fedha taslimu 2,710,000/=, hundi shilingi 1,200,000/= , ahadi
shilingi 10,850,000/=, kiwanja cha kujenga ofisi za Jeshi la Zimamoto chenye
thamani ya shilingi 8,000,000/= na mabati yenye thamani ya shilingi 500,000/=
kwaajili ya kujenga banda la kuhifadhia gari hilo, jumla ya thamani yote ni
shilingi 23,260,000/=.
Akiwashukuru wadau wote
na watumishi waliochangia katika harambee hiyo Mhe. Kijuu alimshukuru pia Mkuu
wa kikosi cha Jeshi la Zimamoto nchini Jenerali Thobias Adengenye kwa kuipa kipaumbele Wilaya ya Karagwe kati ya magari 9 nchini
wilaya hiyo pia nayo imepewa gari moja kutokanan na uhitaji mkubwa uliokuwepo.
Mkuu wa Mkoa pia aliwasistiza
wananchi wa Wilaya ya Kargwe kuona umuhimu wa gari la zimamoto na kulifananisha
na jeshi katika nchi yoyote wakati wa amani kwamba wananchi wanaweza kuona kama
jeshi halina kazi na linatumia fedha za bure lakini vita ikitokea kwa siku moja
huleta madhara makubwa sana kwa nchi kama moto unavyotokea na kusababisha
hasara kubwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Karagwe Mhe. Deodatus Kinawilo alisema kuwa alimua kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la
Zimamoto nchini (Jijini Dar es Salaam)
kuomba gari la zimamoto baada ya kupata taarifa kuwa kulikuwa na magari tisa
(9) yaliyokuwa yameletwa nchini baada ya wilaya yake kukumbwa na janga la moto
katika mji mdogo wa Kayanya na kuunguza soko kuu ambapo vibanda 117 viliungua na kuteketea mapema
mwaka huu 2016.
Matukio makubwa ya moto
yaliyowahi kuikumba Wilaya ya Karagwe tangu mwaka 2014 ni shule ya Sekondari ya
St. Peter Clever bweni liliungua na kuteketea, mwaka 2015 Shule ya Sekondari
Kayanga bweni la wavulana liliungua na kuteketea, mwaka 2016 vibanda 117 vya
soko kuu la Kayanga viliteketea kwa moto pamoja na makanisa mawili kuchomwa
moto.
No comments:
Post a Comment