Baada ya Mwanamitindo anaefahamika kama Binta Diamond Diallo kudai kuwa ana ujauzito wa Mwanamuziki Wizkid mapema January mwaka huu ambapo kwenye interview kadhaa staa huyo wa Afro-Pop kutoka nchini Nigeria alikanusha madai hayo,hatimaye mrembo huyo mara baada ya kujifungua May 31 mwaka huu,aliamua kuweka hadharani majibu ya vipimo vya vinasaba (DNA)kupitia account yake ya instagram ambapo majibu ya vipimo hivyo yanaonesha kuwa mtoto huyo wa kiume ni mtoto halali wa Wizkid.
Mwanamitindo huyo mzaliwa wa Guinea mwenye makazi yake nchini Marekani alipost majibu ya vipimo hivyo akiambatisha na ujumbe uliosomeka “Read between the lines #DNADOESNTLIE #notjustarumor #facts,”.Aliandika.
Hata hivyo Wizkid ambae tayari ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano nax-girlfriend wake Oluwanishola,hajazungumza chochote baada ya mrembo huyo kuweka hadharani majibu hayo ya DNA,japo inadaiwa kuwa Mwanamuziki huyo ameridhia majibu na tayari ameanza kutimiza wajibu wake kama baba.
Kwa sasa Wizkid yupo kwenye maandalizi ya music tour yake na Mwanamuziki Chris Brown inayofahamika kama “One Hell Of A Night”.
No comments:
Post a Comment