Halmashauri ya Wilaya
ya Karagwe yatengeneza nafasi za ajira kwa wananwake na vijana kwa kutengeneza
mizinga ya nyuki 1000 na kuigawa kama mikopo kwa vikundi arobaini vya vijana na
wanawake kwa ajili ya kuzalisha asali na kujiajili ili kupunguza tatizo la ajira katika
wilaya hiyo.
Mizinga 1000 ambayo
tayari imetengenezwa yenye thamani ya shilingi milioni 70 iligawiwa kwa vikundi
40 vya vijana na akina mama kila kikundi mizinga 25 na zoezi hilo la ugawaji wa
mizinga hiyo lilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum
M. Kijuu Juni 8, 2016 katika Halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa ya
utengenezaji wa mizinga hiyo Kaimu Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Ashura Kajuna (Afisa
Uchaguzi) alisema kila kikundi kitakopeshwa mizinga 25 na vikundi hivyo 40
vitapewa kipindi cha neema (Grace Period) ya miezi 12 aidha mikopo hiyo ya
mizinga itarejeshwa ndani ya muda miezi 24 kwa kuzingatia ufaugaji wa nyuki.
Aidha, Bi Ashura
alisema ili kikundi kikidhi vigezo vya kupatiwa mkopo wa mizinga hiyo lazima
kiwe kimesajiliwa na Halmashauri na taasisi nyingine za Serikali, kikundi
lazima kiwe cha wanawake au vijana pia kiwe na uzoefu wa ufugaji wa nyuki na
maeneo ya kufugia yenye malisho yenye malisho ya kutosha (Bee fodders)
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu
aliishukuru Halmashauri ya Wilaya Karagwe kwa kutengeneza mizinga 1000 na
kuwaasa vijana kuchangamkia fursa hiyo ya ajira ili wajiingizie kipato kwa
kufuga nyuki na kuzalisha mazao yake kama asali ambayo alisema ina soko kubwa
ulimwenguni pote. Pia alisema kuwa huo ni mradi mzuri hasa kwa kutunza
mazingira kwani nyuki wakifugwa miti
haitakatwa hovyo hovyo.
Mama Victoria Clemence
ni mwanakikundi wa kikundi cha Wanambingu cha Kayanga ambaye alipokea mizinga
25 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa uzinduzi kwaniaba ya wanakikundi wenzake
alisema kikundi chao tayari wameanza kunufaika na ufugaji wa nyuki kwani tayari
wameanza kuuza asali na kujiingizia kipato, aidha, mizinga hiyo 25 itaongeza
uzalisha wa asali na kukuza kipato cha kikundi chao.
Katika hatua nyingine
Kampuni ya National Beekeeping Supplies Ltd iliyopewa tenda ya kutengeneza
mizinga 1000 na Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kupitia kwa Mkurugenzi wake mkuu Bw. Kaizilege Daudi ilitoa vifaa vya kulina
asali vyenye thamani ya shilingi 2,125,000/= ili kuvisaidia vikundi
vilivyokopeshwa mizinga kulina asali yenye ubora.
Vikundi vilivyogawawi
mizinga ya mkopo vinatemea kunufaika kwa
uzalishaji wa asali kwa wastani
wa kila mzinga kwa msimu ( mwaka mmoja) kuzalisha lita 10 za asali na
kikundi kimoja kinapatiwa mizinga 25, ambapo
wastani wa bei ya asali kwa lita moja ni shilingi 8,000/= (10x25x8,000/= =
2,000,000/=) Kwahiyo kila kikundi kimoja kila mwaka kitakuwa kinaingiza
shilingi 2,000,000/= kwa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment