Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika ya Mashariki (EALA), wameeleza kuunga mkono
jitihada za Rais John Magufuli,kupambana na rushwa na kurejesha uwajibikaji
serikalini huku wakimuomba kukutana nae.
Wakichangia hotuba ya Rais
Magufuli, iliyosomwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao cha tano cha
bunge hilo,kilichofanyika Machi 8 mwaka huu, jijini Dar es salaam, wabunge hao
walisema vita dhidi yaRRushwa inayofanywa na Rais Magufuli iguse pia jumuiya
hiyo.
Mbunge Mike Sebalu kutoka Uganda, alisema Rais Magufuli tangu
amechaguliwa amejitahidi kufanya mambo makubwa kwa taifa la Tanzania ikiwamo
vita dhidi ya rushwa na kurejesha uwajibikaji katika serikali yake.
Hata
hivyo, aliwaomba wabunge wa Tanzania, kuliwezesha EALA kukutana na Magufuli,
ili kujadiliana mwenendo wa jumuiya hiyo.
Mbunge Shyrose Bhanji wa
Tanzania, alisema kasi ya Rais Magufuli, imekuwa na manufaa makubwa sio kwa
watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya Afrika ya
Mashariki.
"vita dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais
Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na
bunge hilo"alisema
Mbunge Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais
Magufuli ambaye ni mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio
vibaya jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na
rushwa.
"Rais Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge
tunamuuunga mkono ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki
mataifa yote yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema.
No comments:
Post a Comment