Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika sekta
ya mawasiliano hadi kufikia kuwa kwenye kundi la nchi zilizoendelea
kimawasiliano Duniani.
Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania takribani
milioni 39 wana laini za simu za kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti
takribani milioni 20 ambapo miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani
zilikuwa 2,963,737.
Haya ni maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania
kuwa nchi bora kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alisikika akisema kwamba,"Ukuaji wa kasi
wa sekta ya mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya
wananchi kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la
Taifa".
Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria,
kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za
mawasiliano.
Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe
Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kazi nzuri
wanazozifanya.
TCRA wana jukumu la kusimamia shughuli hizo
zote wakishirikiana na wadau wa mawasiliano nchini katika kusimamia na
kuzitekeleza kwa makini sera,sheria na kanuni hizo ili kuwezesha kupatikana kwa
huduma za mawasiliano nchini kote kwa kushawishi uwekezaji ,kusimamia vizuri
ushindani pamoja na kutoa fursa sawa kwa watoa
huduma.
TCRA inaendelea kuhakikisha kuwa rasilimali
adimu zikiwemo za masafa na namba za simu zinatumika kwa makini ili kukidhi
mahitaji ya Taifa na maendeleo ikiwa ni kutekeleza lengo la Serikali la
kuwawezesha wananchi wote kupata habari na kuhakikisha hawaachwi nyuma katika
maendeleo ndani ya karne hii ya utandawazi.
Huduma hizi za mitandao pia zimegawanyika
kutokana na kutofautiana kwa mahitaji ya wananchi. Kwa mujibu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, huduma za mitandao ni kama ifuatavyo; Intaneti, Benki
Mtandao, Elimu Mtandao, Matibabu Mtandao,Biashara Mtandao, Malipo Mtandao pamoja
na Mawasiliano Mtandao.
Huduma hizi zimekuwa zikirahisisha mambo mengi
hasa ya kikazi na ya kijamii,ukiangalia kwa sasa ofisi zote za umma na za
binafsi wanatumia huduma za mitandao katika kufanya shughuli zao zote za kiofisi
kama njia salama ya kuhifadhi data zao.
Kwa ofisi za Serikalini wameipa huduma hii jina
la Serikali Mtandao (E-Government) ambapo watumishi wa umma wanashauriwa kutumia
mtandao huu ili kuhakikisha kazi zote za ofisi zinafanyika katika hali ya
usalama na usiri mkubwa.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Mllao anasisitiza umuhimu wa watumishi wa
Umma kupata mafunzo ya huduma za mitandao ili kuepuka matatizo yanayotokana na
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu
yao.
“Tumegundua kwamba watumishi wanahitaji muongozo
juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo tunashkuru sana uongozi wa
TCRA kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wetu,”alisema Bi.Nuru wakati wa
mafunzo ya watumishi kuhusu masuala ya
mawasiliano.
Kwa upande mwingine, jamii inatumia huduma za
mitandao kwa ajili ya mawasiliano kupitia intanenti ambapo kama tulivyosema hapo
awali jumla ya wananchi milioni 20 wanatumia huduma za intanenti ambazo
zinahusisha matumizi ya mitandao ya kijamii kama ya facebook, instagramu,WhatsApp, Forums,
Linkedin pamoja na barua pepe katika
kuwasiliana kati ya mtu mmoja na mwingine.
Matumizi hayo ya mitandao ya kijamii pia ni
muhimu kwa wananchi kwa kuwa inatumika kama njia rahisi katika kupashana habari
kwa haraka na kufanya dunia kuonekana kama kijiji kwani watu hupata habari za
masafa ya mbali kwa haraka.
Kama tunavyojua "Kizuri hakikosi kasoro",
japokua matumizi ya huduma za mitandao yana faida nyingi lakini kuna baadhi ya
madhara hutokea kama mitandao hiyo ikitumiwa
vibaya.
Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy
anasema kuwa ongezeko la watumiaji wa huduma za mawasiliano linaenda sambamba na
ongezeko la vifaa mbalimbali vinavyowezesha mawasiliano hayo
kufanyika.
"Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na simu za
kiganjani,vifaa vya mawasiliano ya kiganjani (tablets), kompyuta pamoja na
modemu, kadri idadi ya watu na vifaa vya mawasiliano vinavyoongezeka ndivyo
matumizi mabaya ya mitandao yanazidi kuibuka,"anasema
Mungy.
Kuna baadhi ya wananchi ambao tunaweza kusema
hawana maadili ya kutosha ambao wanatumia vibaya huduma hizi za mitandao kwa
ajili ya kujinufaisha kwa njia zisizo za halali pamoja na kuupotosha umma kwa
kutuma vitu ambavyo viko kinyume na maadili ya
mtanzania.
Matumizi mabaya ya mitandao yanapelekea kuwepo
kwa madhara kama ya mauaji, wizi, ukiukwaji wa maadili, ugomvi na kutokuelewana
katika jamii zetu.
Ili kuzuia madhara haya ni lazima kila mmoja
azingatie matumizi sahihi ya huduma za mitandao. Mamlaka inayosimamia Huduma za
Mawasiliano nchini imeelezea baadhi ya mambo muhimu ambayo yatasaidia kuimarisha
usalama pindi utumiapo huduma hizo.
Unatakiwa kutotumia nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja
wala kuweka nywila ambazo mambo yako binafsi ambayo yanajulikana kwa watu wengi
ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia katika mtandao wa mtu
mwingine.
Unashauriwa kubadilisha nywila mara kwa mara
pamoja na kutengeneza nywila ambayo ina muunganiko wa namba na herufi ili isiwe
rahisi mtu mwingine kuibuni pia nywila ni siri yako hushauriwi kumpa mtu
mwingine yoyote.
Aidha, hutakiwi kuiandika sehemu yoyote kwa
ajili ya kumbukumbu wala kukubali au kujibu barua pepe zinazotoka kwa watu
usiowajua kwa kuwa wanaweza kutumia kama njia ya kufahamu nywila yako.
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania inawasisitiza
wananchi kujifunza njia bora za kutumia mawasiliano hususani matumizi mazuri ya
mitandao ya kijamii ili iweze kuwanufaisha na kuendelea kukuza uchumi wa nchi
kuliko kuitumia vibaya hatimaye ikaleta madhara ambayo yatasababisha matatizo
kwa mtu binafsi au Taifa kwa ujumla.
Watanzania tunatakiwa kubadilika kulingana na
hali halisi ya maendeleo ya nchi yetu ambapo kwa sasa teknolojia ya huduma za
mitandao inazidi kukua kwa kasi hivyo kurahisisha zaidi huduma
muhimu.
Huduma hizi za mitandao ni kwa ajili ya wananchi
wote, hatutakiwi kuziacha zitupite kushoto

No comments:
Post a Comment