BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA LIVE

Wednesday, May 25, 2016

MATUKIO YA BUNGE NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani wakifuatilia hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na Majibu.
 Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment