Shirika la
Umeme Tanzania limewataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi
ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini Mhandisi
Majige Mabulla wakati wa mkutano na
vyombo vya habari.
Majige
amesema kuwa moto hauwezi kutokea endapo
mtumiaji wa umeme atahakikisha kuwa mfumo wa umeme katika nyumba yake umesukwa
na fundi ama mkandarasi aliyesajiliwa.
“Kuwa makini
katika matumizi bora ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi,hita za
umeme,kuchaji simu,kompyuta kutasaidia kupunguza au kuondoa tatizo la majanga
ya moto” alisisitiza Mabulla.
Akizungumzia
hatua nyingine zinazoweza kusaidia kuzuia majanga ya moto Mhandisi Majige amesema ni kuepuka kuweka vitu vinavyoweza
kushika moto kirahisi, karibu na nyaya ama maungio ya nyaya za umeme ndani ya
nyumba .
Majige
alitoa wito kwa watumiaji wa umeme kutoa taarifa pale wanapotaka kuongeza
matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa ndani ya makazi ya watu, ili tathmini ya
uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji yaliyoongezeka ifanyike.
Katika
kuzuia matukio ya moto TANESCO imekuwa ikihakikisha kuwa inamfikishia mteja umeme
ulio salama na usiokuwa na madhara kwa mtumiaji, kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye
mita.
Kwa kipindi
kirefu sasa kumekuwepo na matukio ya ajali za moto katika makazi ya watu ambayo
yamekuwa yakisababisha madhara, ikiwemo
kusababisha vifo,majeruhi na uharibifu
wa mali.
No comments:
Post a Comment