Achilia mbali performance nzuri aliyofanya Rihanna wakati wa utoaji wa tuzo za Billboard Music Awards 2016,issue iliyotrend kuhusu mrembo huyo ambae album yake ya “Anti” imevunja rekodi na kuwa double platinum ilikua ni pete aliyoonekana ameavaa kwenye mkono wake wa kushoto.
Kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood life,mtu wa karibu kutoka kwenye tour team ya Rihanna amedai kuwa engagement ring aliyoonekana nayo Rihanna kwenye tuzo za Billboard alipewa kama zawadi na rapper Drake huku pete hiyo(16 carat diamond ring) ikikadiriwa kuwa na thamani ya kiasi cha dola milioni 1.
Hata hivyo Rihanna na Drake wanadaiwa kupanga mahusiano yao yabaki kuwa siri mpango ambao wanaamini kuwa utakua na manufaa ya kibiashara kwenye shughuli zao za kimuziki as we know wamekua wakishirikishana kwenye baadhi ya single kila wanapotoa album mpya. “Drake is Robyn’s man,He’s not with anyone else, and neither is she,but trust me both of them they love each other,actually they got some plan but they dont give sh**t on public”.Kilidai chanzo hicho cha habari.
Sio mara ya kwanza kwa rapper Drake ambae album yake ya “Views”inazidi kufanya vizuri kumzawadia Rihanna pete kwani mnamo mwaka 2014 wakiwa kwenye tour jijini London nchini Uingereza rapper huyo mzaliwa wa Toronto,Canada alionekana akivinjari na Rihanna ambapo taarifa zilivuja kuwa alimzawadia yellow diamond ring yenye thamani ya kiasi cha dola elfu arobaini na mbili ($42,000) hivyo kitendo cha rapper huyo kumzawadia Rihanna $ 1million dollar diamond ring kinatafsiriwa kuwa pengine wawili hao ni wapenzi wenye mipango mikubwa zaidi ya kimaisha.
No comments:
Post a Comment