BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA LIVE

Friday, August 12, 2016

MISAADA HUWA HAITOZWI KODI – TRA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya utozwaji wa kodi zamisaada inayotolewa na wadhamini kusaidia Sekta ya Maendeleo yaMichezoNchini.

Ufafanuzi huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa MlipaKodi, Richard Kayombo kutokana na habari iliyochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Serikali kukosa mabilioni ya fedha kwa sababu ya kutokukusanya kodi ya fedha zinazotolewa na wadhamini kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Fedha zinazotolewa kama msaada kutoka kwa wadhamini huwa hazikatwi kodi lakini TRA hupata mapato yake kutokana na matumizi ya fedha hizo hasa pale wahusika wanapozitumia katika shughuli za kiuchumi”,alisema Kayombo.

Kayombo ametaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazoweza kuwaingizia mapato kutoka kwenye misaada hiyo kuwa ni; kodi za waajiriwa wakiwemo makocha na wachezaji, makusanyo ya uwanjani ,kupewa huduma za kitaalam pamoja na majengo ya kupangisha au kupanga.

Amefafanua kuwa kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini  (TFF) linakodishajengo basi fedha wanazopata lazima walipe kodi ya asilimia 10 kutoka kwenye fedha hizo na kama wao ndio wamekodi jengo kwa ajili ya matumizi yao wanatakiwa kutoa kodi ya asilimia 5.

Kwa upande wa kodi kutoka kwa waajiriwa, Mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimukwa vilabu vya michezo kuwa michezo ni ajira kama ajira zingine hivyo mishaharayao inatakiwa kukatwa kodi kulingana na kiasi wanacholipwa.

Zoezi la kuwatoza kodi makocha na wachezaji limeanza rasmi mwaka huu.
MWISHO
 
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

SUMATRA KUENDELEA KUKUSANYA MAONI YA WADAU.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa  Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema kuwa bado inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa usafiri wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA, Bw. David Mziray ambaye alibainisha kuwa kwa sasa bado wanaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau kama sheria ya mamlaka hiyo inavyoelekeza kabla ya kuja na kiwango rasmi cha nauli ya usafiri huo.

“Tumetoa muda mpaka Agosti 19 mwaka huu iwe ndio mwisho wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na bei elekezi ya nauli kwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu” Alisema Mziray.

Pia, Mziray alifafanua kuwa kwa kipindi hiki ambacho wanapokea maoni wameielekeza Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) waendelee kutoza nauli ya shilingi 400 kwa watu wazima na shilingi 200 kwa watoto na wanafunzi mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

Alieleza kuwa tangu usafiri huo wa treni uanze huduma zake imeonekana kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri muda mrefu njiani na sasa wanaweza kuwahi katika maeneo yao ya kazi na biashara wakiwemo wanaokwenda kwenye soko la Kimataifa la samaki la Ferry.

Aidha, aliongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya usafiri pasipo na matatizo yoyote kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kuongeza mabehewa kutoka 15 yaliyopo sasa hadi kufikia mabehewa 20.

Akizungumzia baadhi ya changamoto walizoziona tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya usafiri wa Treni alisema kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya vyoo na maji katika baadhi ya vituo.

“Tunatarajia hivi karibuni Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) itajenga vituo vipya na kufanya ukarabati kwenye vituo vya zamani ili kuweza kuwaondolea usumbufu wananchi kwa kuweka huduma mbalimbali ikiwemo vyoo na maji kwenye vituo hivyo” Alisema Mziray.

Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu ilizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hasa wakazi wa maeneo ya  Gongolamboto, Pugu na Chanika.
MWISHO.
Na Abushehe Nondo (MAELEZO).


TTCL YAHAKIKISHA HUDUMA BORA KWA MASHIRIKA NA TAASISI YATAKAYOHAMIA DODOMA



DAR ES SALAAM
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imejipanga kutoa huduma bora kwa mashirika na  taasisi zinazotarajia kuhamia Mjini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano TTCL  Bw. Nicodemus Thom Mushi leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa miaka mitatu wa mageuzi ya kibiashara wa Kampuni hiyo.

Mushi ameeleza kuwa, katika mpango huo TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma ya Serikali ya kuhamia mjini Dodoma kwa kutoa huduma bora kwani tayari kampuni hiyo ina rasilimali watu, vifaa na wataalamu wa kutosha katika kutoa huduma za Mawasiliano.

“Nitumie fursa hii kuwaomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na Taasisi zote kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo zote zimethibitika kuwa ni huduma bora na za uhakika na zenye gharama nafuu,” amefafanua Mushi.

Aidha, kampuni hiyo imeboresha njia ya kusikiliza wateja ambapo hivi sasa malalamiko ya wateja hushughulikiwa ndani ya masaa matatu toka mteja anapotoa taarifa katika kituo cha huduma kwa mteja.

Akiongelea juu ya maboresho, Mushi amesema kuwa, kampuni hiyo imeleta huduma mpya ya 4G LET ambayo inapelekea intaneti yenye kasi zaidi, vile vile imeboresha miundo mbinu ya mitandao ya simu na data na kuondoa mitambo chakavu.

Sambamba na hayo Mushi amewahakikishia wateja kuwa TTCL ni kampuni pekee ambayo ni suluhisho la huduma bora na ya uhakika wakati wote na mahali popote iwe ni nyumbani, sehemu ya kazi na hata kwenye vyombo vya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
MWISHO
Na Georgia Misama – MAELEZO




Thursday, July 21, 2016

SERIKALI YAKINUSURU CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA KCU 1990 LTD MKOANI KAGERA

JENGO LA OFISI KUU YA CHAMA CHA USHIRIKA KCU 1990

Bodi na Meneja Mkuu wa KCU 1990 LTD Wasimamishwa Kazi Kuanzia Sasa
Nafasi ya Mrajisi Msaidizi Kagera yasitishwa na Kuteuliwa Mwingine.
Akaunti zote za KCU 1990 LTD Zasitishwa Kupisha Uchunguzi
Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera, Kagera Co operative Union 1990 LTD
(KCU) pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho na Mrajisi Masidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera wamesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 21.07.2016 kwa tuhuma za ubadhilifu zaidi ya shilingi milioni 900 pamoja na kuingia mikataba yenye harufu ya rushwa iliyopelekea hasara kubwa kwa Chama hicho Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera.
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akitangza rasmi kusimamishwa kwa Bodi ya KCU pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika alisema kuwa Bodi hiyo ikishirikiana na Meneja Mkuu Bw. Vedastus Ngaiza walitoa taarifa za uongo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho wa mwezi Mei 2016 kuhusu deni wanalodaiwa na Benki ya CRDB.
Dkt. Rutabanzibwa alisema baada ya kutuma wakaguzi kutoka ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Wakaguzi hao walibaini kuwa taarifa waliyosomewa wananchama katika mkutano ilitaja kuwa deni lilikuwa Shilingi bilioni 2.8 kumbe haikuwa kweli kwani deni lilikuwa limepanda hadi shilinngi bilioni 3.15 Bodi na Meneja Mkuu walikuwa wamewadanganya wanachama wa chama hicho.
Pili,
Wakaguzi hao waligundua kuwa shilingi Milioni 124 zilitumika katika malipo na hakukuwa na maelezo ya kutosheleza kuhusu malipo ya fedha hizo.
Tatu
, KCU iliingia mikataba ya kukodisha majengo yake amabayo haikufuata bei ya soko kwa sasa, na mikataba hiyo ilifungwa kwa makubaliano ya miaka 10 jambo ambalo linapelekea Chama hicho kulipwa pango kwa bei ya chini kabisa isiyoendana na soko.
Nne
, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU kimekuwa kikinunua kahawa ya kiwango cha chini kabisa na kusababisha hasara kubwa.
Tano
, Chama cha KCU kilijiingiza kataika miradi isiyokuwa na tija kama mradi wa kununua maharage ambao ulikisababishia hasara kubwa Chama hicho.
Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa kutokana na sheria Na. 6 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini Bodi ya KCU hakufanya kazi yake ipasavyo ya kukisimamia vizuri chama hicho Aidha, Bodi hiyo ilifanya vikao 12 kwa mwaka jana 2015 vikao ambavyo vinaonekana havikuwa na tija kwani pamoja na vikao hivyo vya Bodi kufanyika bado kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha.
MAELEKEZO
Dkt. Ruatabazibwa baada ya kutaja ubadhirifu uliofanyika katika Chama Kikuu cha Ushirika KCU alisema kuwa Serikali imeamua kuchuka hatua zifuatazo;
Kufuta Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU iliyoteuliwa mwaka 2014
Kusitisha ajira ya Meneja Mkuu wa KCU Bw. Vedastus Ngaiza mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha utakapokamilika.
Kusitisha nafasi ya Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Bw. Nestory Shorozi kwani ubadhirifu huo ulifanika yeye akiwepo bila kukishauri vizuri Chama hicho Kikuu cha Ushirika .
Akaunti zote za Chama cha Ushirika KCU kusimamishwa mara moja mpaka hapo utaratiibu mzuri utakapokuwa umewekwa .
 
KUNUSURU CHAMA
Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa katika kukinusuru Chama Kikuu cha KCU pia na kuendelea na Msimu wa manunuzi ya kahawa Serikali imefanya uteuzi mdogo wa Mrajisi Msaidizi Bw, Robert Makene Mtambo kutoka Ukerewe Mkoani Mwanza atakayeshikiria kwa muda nafasi ya Bw. Nestory Shorozi aliyekuwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera.
 
Aidha mrajisi Msaidizi aliyeteuliwa Bw. Mtambo atakaimu nafasi ya Meneja Mkuu wa KCU iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Vedastus Ngaiza. Katika kukaimu nafasi hiyo Bw. Mtambo atatakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama wa KCU ndani ya mwezi mmoja na katika mkutano huo atateuliwa Mwenyekiti ambaye atatakiwa kusoma taarifa halisi ya KCU iliyotakiwa kusomwa mwezi Mei 2016 katika Mkutano Mkuu.
Adha Dkt. Rutabanzibwa alisema Serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo bali ilifanya uchunguzi wa kutosha ikiwa ni pamoja kuipa bodi nafasi ya kujieleza lakini haikutoa maelezo ya kutosha na badala ya kupunguza deni wao waliliongeza deni likapanda zaidi. Pia Dkt. Rutabanzibwa aliviagiza vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU, Polisi na Usalama kuanza kulifanyia kazi suala hilo mara moja.
Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa alimalizia kwa kusema kuwa Serikali imeamua kulifanyia kazi suala la VyamaVikuu vya Ushirika nchini kwani vyama hivyo vimeonekana kuwa badala ya kuwasaidia wakulima vinawadidimiza ambapo alisema walianzia Mwanza, sasa Kagera, na wanaelekea Mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga.

Tuesday, June 28, 2016

PICHA:Rapper Birdman na Toni Braxton waamua kuweka wazi hisia zao za kimapenzi.



Wakati wa utoaji wa tuzo za muziki za BET mwaka huu yalijiri matukio mengi nyuma ya pazia,miongoni mwa matukio hayo ni muendelezo wa tetesi zilizozagaa mitandaoni kuwa Birdman,rapper na mmiliki wa music label ya  Cash Money Records kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na staa wa miondoko ya Pop na R&B,Toni Braxton.
toni braxton 000pMashuhuda wameuambia mtandao wa TMZ,kuwa wakati zoezi la utoaji tuzo za BET likiendelea,wawili hao walionekana pamoja backstage wakishikana mikono huku wakionekana watu wenye hisia za kimapenzi.
“Toni and Birdman spent some time together backstage,”…..“They were holding hands,talk closed to each other”…”it seems they had same feelings”.Mashuhuda waliuambia mtandao huo.
                     Birdman & Toni Braxton @BET,Award 2016.
Ingawa wawili hao hawajazungumza chochote juu ya tetesi hizo,Mama mzazi wa Toni Braxton anaefahamika kwa jina moja la Evelyn,ameuambia mtandao wa Us Magazine kuwa hajali watu wanamzungumziaje Birdman na haoni tatizo kwa mwanae kuwa kwenye mahusiano na rapper huyo.“I don’t care what others say about him. He is a nice man. He is full of respect.”…”Ever since I’ve been knowing that man, he’s been phenomenal”.Alidai Mama mzazi wa Toni Braxton.
Tetesi za Birdman (41) na Toni Braxton (48) kuwa na mahusiano ya kimapenzi zilianza kuenea mitandaoni baada ya show ya Toni Braxton jijini Atlanta mnamo June 2,2016 baada rapper Birdman kujumuika nae alipopanda jukwanii ambapo wakati mmiliki huyo wa music label ya Cash Money Records anashuka  jukwaani Braxton alitamka kwa sauti akitumia kipaza sauti “Respect that man y’all”.Alitamka mwanamuziki huyo.