|
DAR
ES SALAAM
Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) imejipanga kutoa huduma bora kwa mashirika na
taasisi zinazotarajia kuhamia Mjini Dodoma.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano TTCL Bw. Nicodemus Thom Mushi leo Jijini
Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa
miaka mitatu wa mageuzi ya kibiashara wa Kampuni hiyo.
Mushi
ameeleza kuwa, katika mpango huo TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma ya
Serikali ya kuhamia mjini Dodoma kwa kutoa huduma bora kwani tayari kampuni
hiyo ina rasilimali watu, vifaa na wataalamu wa kutosha katika kutoa huduma
za Mawasiliano.
“Nitumie
fursa hii kuwaomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na Taasisi zote
kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo zote zimethibitika kuwa ni huduma
bora na za uhakika na zenye gharama nafuu,” amefafanua Mushi.
Aidha,
kampuni hiyo imeboresha njia ya kusikiliza wateja ambapo hivi sasa malalamiko
ya wateja hushughulikiwa ndani ya masaa matatu toka mteja anapotoa taarifa
katika kituo cha huduma kwa mteja.
Akiongelea
juu ya maboresho, Mushi amesema kuwa, kampuni hiyo imeleta huduma mpya ya 4G
LET ambayo inapelekea intaneti yenye kasi zaidi, vile vile imeboresha miundo
mbinu ya mitandao ya simu na data na kuondoa mitambo chakavu.
Sambamba
na hayo Mushi amewahakikishia wateja kuwa TTCL ni kampuni pekee ambayo ni
suluhisho la huduma bora na ya uhakika wakati wote na mahali popote iwe ni
nyumbani, sehemu ya kazi na hata kwenye vyombo vya usafiri kutoka sehemu moja
kwenda nyingine.
MWISHO
Na
Georgia Misama – MAELEZO
|
Friday, August 12, 2016
TTCL YAHAKIKISHA HUDUMA BORA KWA MASHIRIKA NA TAASISI YATAKAYOHAMIA DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment