Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya utozwaji wa kodi zamisaada
inayotolewa na wadhamini kusaidia Sekta ya Maendeleo yaMichezoNchini.
Ufafanuzi huo
umetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa MlipaKodi, Richard Kayombo
kutokana na habari iliyochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu
Serikali kukosa mabilioni ya fedha kwa sababu ya kutokukusanya kodi ya fedha
zinazotolewa na wadhamini kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
“Fedha
zinazotolewa kama msaada kutoka kwa wadhamini huwa hazikatwi kodi lakini TRA
hupata mapato yake kutokana na matumizi ya fedha hizo hasa pale wahusika
wanapozitumia katika shughuli za kiuchumi”,alisema Kayombo.
Kayombo ametaja
baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazoweza kuwaingizia mapato kutoka kwenye
misaada hiyo kuwa ni; kodi za waajiriwa wakiwemo makocha na wachezaji,
makusanyo ya uwanjani ,kupewa huduma za kitaalam pamoja na majengo ya
kupangisha au kupanga.
Amefafanua kuwa
kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) linakodishajengo basi
fedha wanazopata lazima walipe kodi ya asilimia 10 kutoka kwenye fedha hizo na
kama wao ndio wamekodi jengo kwa ajili ya matumizi yao wanatakiwa kutoa kodi ya
asilimia 5.
Kwa upande wa
kodi kutoka kwa waajiriwa, Mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimukwa vilabu vya
michezo kuwa michezo ni ajira kama ajira zingine hivyo mishaharayao inatakiwa
kukatwa kodi kulingana na kiasi wanacholipwa.
Zoezi la
kuwatoza kodi makocha na wachezaji limeanza rasmi mwaka huu.
MWISHO
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
No comments:
Post a Comment