Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akihutubia
mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini
Geneva-Uswisi
……………………………………………………………………………………..
Mwandishi
maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo
yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto Ummy
mwalimu wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini
Geneva,Uswisi.
Ummy
alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua
katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo 54 kati ya
vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha,
mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania
imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa
polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa
watoto.
“Ninaeleza
kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini
Tanzania ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia
21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia wizara ya
afya itaimarisha na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na
ugonjwa huu”alisema
Kwa
upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza
maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa
upande wa Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa hadi kufikia asilimia
0.6 .
Katika
kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga na
kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia kila mtanzania popote
alipo, “ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi
katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na
kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya
nchini”.
Waziri
Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia kuwasilisha
muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa
na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi katika
kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha au kutokuwa na fedha
kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.
Mkutano
mkuu wa mwaka wa Afya Duniani hufanyika nchini Geneva –Uswis kila mwaka mwezi
mei ambao huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la
afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na taasisi zinazoshiriki
katika kutoa huduma za afya Duniani.Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya
Tanzania bara Mhe.Ummy mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud
Kombo.
Posted by Williammalecela.com
No comments:
Post a Comment