BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA LIVE

Monday, June 27, 2016

VIDEO:Beyonce na Kendrick Lamar walivyoamua kupinga ubaguzi kupitia colabo yao ya “Freedom”.




Jumapili ya tarehe 26 June ilikua ni siku maalum ya utoaji wa tuzo za BET zinazoandaliwa na kituo kikongwe cha burudani nchini Marekani  cha Black Entertaiment Televison (BET),mbali na utoaji wa tuzo hizo wasanii mbalimbali wali-perfom na kukata kiu ya maelfu ya watazamaji waliohudhuria utoaji wa tuzo hizo kwenye ukumbi wa Microsoft Theater,huko Las Vegas.
Miongoni mwa pefromance zilizowashangaza wengi ni pale Pop and R&B hit maker Beyonce alipopanda jukwaani na ku-perfom single yake inayofahamika kama  “Freedom”aliyomshikirisha rapper Kendrick Lmar,wimbo ambao maudhui yake yamejaa hisia zenye mrengo wa kisiasa kutokana na kuripotiwa matukio mengi ya mauaji ya watu weusi yaliyofanywa na polisi nchini Marekani kwenye miaka ya hivi karibuni.
beyonce and kendrick 009Kwa kuthibitisha hilo hata wakati ma-dancer wa Beyonce wanapanda jukwaani walisindikizwa na sauti ya Mwanaharakati wa haki za binadamu duniani,Hayati Martin Luther King Jr ambapo sehemu ya hotuba yake maarufu iliyopewa jina “I Have A Dream”ilisikika.
Wimbo huu unapatikana kwenye album mpya ya Beyonce inayofahamika kama ‘Lemonade’.

No comments:

Post a Comment