Rapa namba moja Afrika Mashariki kwa sasa AY, amesema kitu anachokikazania kwa sasa katika maisha yake ni masomo ambayo yatamuwezesha kuwa Rubani na kufanikiwa kurusha Ndege siku za Usoni.
Hit maker huyo wa ‘Zigo’ amesema kurusha Ndege ndio kitu pekee anachokikazania kwa sasa katika maisha yake ili akamilishe ndoto zake.
“Nataka kurusha Ndege icho tu ndio ninachokikazania kwa sasa, nataka nitimize ndoto zangu nikifanikiwa moyo wangu utaridhika mno” Alisema.
Katika hatua nyingine AY, alifunguka jambo ambalo watu wengi hawalifahamu kuhusu rapa mwenzie wa Kenya Prezoo kuwa ni Rubani aliyekamilika katika mafunzo ya kurusha Ndege.
“Prezoo ni rubani kabisa yani kakamilika, mbona Kenya wana wengi tu wanarusha Ndege alafu wanafanya vitu vingine, unajua Ndege ni kama gari tu, Bongo tu ndio bado kama kipindi kile simu zinaingia” Alisema AY.

No comments:
Post a Comment