Kwenye show hiyo iliyofanyika New York City @Irving Plaza on May 25 inadaiwa kuwa milio ya risasi ilianza kusikika mara baada ya rapper Maino na msanii mwingine anaefahamika kama Uncle Murda kuperfom ambapo katika tukio hilo mtu mmoja aliuawa huku watu wengine wannee wakijeruhiwa akiwemo rapper T.I kama ilivyoripotiwa na kituo cha Tv cha ABC7 New York.
T.I mwenye umri wa miaka 35 kupitia akaunti yake ya instagram alitoa pole kwa familia ya marehemu na wote waliojeruhiwa katika tukio hilo. “My heartfelt condolences to the family that suffered the loss & my prayers are with all those injured. Respectfully, Tip.”aliandika rapper huyo.Hata hivyo mtu mmoja anaefahamika kama Troy Ave anashikiliwa na polisi jijini New York baada ya video iliyovuja mtandaoni ikionsesha kuwa yeye ndie aliekua kifyetua risasi hizo.
Rapper Troy Ave,Mshukiwa wa mauaji hayo.
Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la New York Times Taroy Ave ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Ronald Mc Phatter anadaiwa kufikia uamuzi huo huku mlengwa mkuu akiwa ni rapper Maino,mara baada ya Maino kutopanda nae jukwaani kuperfom na badala yake akapanda stejini na rapper Uncle Murda ambapo katika ufyetuaji huo wa risasi ulipelekea watu wanne kujeruhiwa na kusababisha kifo cha Ronald MC Phatter ambae alikua rafiki na mlinzi wa rapper Troy Ave.
No comments:
Post a Comment