Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya Kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali
wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa
Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Kaimu
Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea
wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya
Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi
wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na
wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi
kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi
wenye nia ya kuwakwamisha.
Baadhi
ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka
wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo
aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi
mbalimbali za ujenzi nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi
ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya
Usajili ya Makandarasi (CRB).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha
kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi
(CRB).
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
|
No comments:
Post a Comment