BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA LIVE

Wednesday, May 25, 2016

Kanali mstaafu wa jeshi auawa Burundi.

Taifa la Burundi limekumbwa na mauaji tangu rais Pierre Nkurunziza kuponea jaribio la mapinduzi na mandamano ya kumtaka aondoke madarakani baada ya kuongoza kwa miaka kumi.

Mapema jioni hii kanali mmoja wa kijeshi aliyestaafu ameuawa kwa kupigwa risasi huku mwanawe akijeruhiwa kwenye shambulizi la hivi punde katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.

Kwingineko jana usiku, watu waliokuwa na silaha walimuua polisi na raia mmoja katika wilaya ya Ndava iliyo eneo la Mwaro nchini humo.
Kanali mmoja wa kijeshi aliyestaafu ameuawa kwa kupigwa risasi huku mwanawe akijeruhiwa kwenye shambulizi la hivi punde katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.

No comments:

Post a Comment